Mara nyingi taarifa ya jambazi kuuwawa na mwanaume ni kitu cha kawaida lakini kwa jambazi kuuwawa kwa risasi iliyopigwa na mwanamke tena bibi mwenye umri wa miaka 61 anaekaribia 62 ni kitu kikubwa sana.
Jumapili december 9 2012 nilisafiri mpaka Bagamoyo kufanya mahojiano na bibi ambae ijumaa iliyopita alivunja rekodi ya stori za ujambazi kuingia kwenye habari kutokana na kumuua jambazi mmoja kati ya nane waliomvamia nyumbani kwake, baada ya kumuua huyo mmoja wale wengine waliobaki wakakimbia.
Picture by Millard Ayo
No comments:
Post a Comment