Thursday, December 13, 2012

KAULI YA CHADEMA KUHUSU MAGUFULI KUMPIGIA KAMPEN ODINGA

Mwenyekiti wa chama cha demokrasia CHADEMA kimeitaka Serikali kutolea ufafanuzi suala la WazirI wa ujenzi Dr. John Magufulu kuhudhuria Sherehe za kutambulishwa kwa mgombea urais chama cha ODM Kenya Raila Odinga endapo suala hilo lina uhusiano wowote wa Kiserikali.

Mkurugenzi wa mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa Ezekiel Wenje amesema kitendo cha waziri huyo kuhudhuria sherehe za kutambulishwa wa Raila kinatoa picha mbaya ya serikali ya Tanzania na Serikali ya Kenya iliyopo Madarakani kutokana na ushirikiano wa muda mrefu kati ya serikali hizo.

kwenye sentensi nyingine Wenje amesema Magufuli kupanda jukwaani kuanza kumnadi kiongozi wa ODM ni ukiukwaji wa kanuni na taratibu za kimataifa ambapo amedai kwa mujibu wa kanuni za Umoja wa Mataifa ni kosa kubwa kuingilia siasa za nchi nyingine hata kama kunamahusiano baina ya nchi hizo mbili

No comments: